Wednesday, 25 November 2015

MZOZO WA SUDAN KUSINI.


Image captionWapiganaji Sudan kusini
Viongozi wa pande zinazopingana Sudan, hawajaunda serikali ya mpito katika kipindi cha siku 90 kama ilivyokubaliwa mwezi wa 8.
Marekani imeonya kwamba mpango huo wa amani utapata ufumbuzi pale serikali hiyo ya mpito itakapoanzishwa.
Imesema mapigano yamekuwa yakiendelea kila siku na hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya.
Maelfu ya watu wameuawa tangu Rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar walipovurugana Desemba mwaka 2013.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imezitaka pande zote kushiriki mkutano wa kwanza wa pamoja utakaofanyika siku ya Jumamosi mjini Juba.

No comments:

Post a Comment