Rais wa Gambia, Yahya Jammeh,amepiga marufuku tohara ya wanawake nchini humo akisema inakwenda kinyume na mafundisho ya kiislamu.
Watabibu wamekuwa wakieleza matatizo ya kiafya yanayotokea kutokana na tabia hiyo lakini hilo halijapunguza visa vya upashaji tohara wanawake nchini hiumo.
Sasa rais Yahya Jameh amesema amekuwa akitafiti kwa muda wa miaka 21 katika kitabu tukufu cha Quran na vilevile kupitia mahojiano na wanazuoni wa kiislamu na hamna ushahidi wowote wa kufungamanisha kitendo hicho na dini ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment