Wednesday, 25 November 2015

FARAGHA:FACEBOOK YASHTAKIWA UBELGIJI.


Image copyrightGetty
Image captionFacebook
Uamuzi unaotaka mtandao wa facebook kufanya mabadiliko muhimu katika mazingira yake ya faragha nchini Ubelgiji umecheleweshwa huku nakala za mahakama zikitafsiriwa kiingereza ,BBC imebaini.
Kesi hiyo iliowasilishwa na tume ya faragha nchini Ubelgiji BPC inautaka mtandao huo kutowafuatilia watu wasiotumia mtandao huo haraka iwezekanavyo la sivyo ipigwe faini.
Uamuzi huo ulitolewa mnamo mwezi Novemba huku mtandao wa facebook ukipewa saa 48 kuafikia masharti ya uamuzi huo.
Hatahivyo facebook imesema kuwa inajadiliana na tume hiyo ya kukabiliana na maswala ya faragha nchini Ubelgiji BPC.
''Tulikutana na BPC na kuwapatia suluhu kuhusu baadhi ya maswala yanayowatia wasiwasi kuhusu mazingira yetu ya faragha.Tunatumia data hizi ili kuweza kuzuia jaribio la kuzichukua zaidi ya akaunti 33,000 nchini Ubelgiji katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita,na data kama hizo hutumiwa na wahudumu wengine wa mitandao.Tunatumai kwamba tutasuluhisha tatizo hili bila kuhatarisha uhuru na usalama wa watu wanaotumia facebook'',alisema Alex Stamos,ambaye ni fisa mkuu wa usalama katika mtandao huo.
Msemaji wa BPC ameiambia BBC kwamba uamuzi huo ulifaa kuwasilishwa rasmi kwa facebook kwa kuwa unangojea kutafsiriwa kiingereza katika kurasa 33.
Kesi hiyo inahusu data inayotumia na facebook kuwafutilia kwa miaka 5 wasiotumia mtandao huo.

No comments:

Post a Comment