Wednesday, 25 November 2015

WENGER:TUNA MATUMAINI YA KUFUZU.


Image copyrightEPA
Image captionWenger
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ana imani kwamba klabu yake itafuzu katika kundi la vilabu 16 katika kombe la vilabu bingwa Ulaya baada ya kujiweka katika hali ya ushindi wa lazima dhidi ya Olympiakos.
Arsenal iliishinda Dinamo Zagreb katika uwanja wa Emirates siku ya jumanne huku Bayern Munich ikiicharaza Olympiakos 4-0.
Hii inamaanisha kwamba Arsenal itahitaji ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Olympiakos ama ushindi wowote wa kuanzia mabao matatu ili kuiweka Arsenal katika makundi ya timu 16 bora.
Image copyrightReuters
Image captionWenger
Wenger:Tulihitajika kutoka katika mechi hii tukiwa na fursa na tumefanya hivyo,sasa wacha turekebishe kile tulichokosea kufikia sasa.
Arsenal ilishindwa na Olympiakos 3-2 nyumbani na sasa iko katika nafasi ya hatari baada ya kushindwa na Dinamo Zagreb na Bayern.

No comments:

Post a Comment