Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya New Zealand ya mchezo wa raga Johan Lomu amefariki dunia.
Risala za rambirambi zimeendelea kutumwa kutoka kila pembe duniani.
Lomu alifanyiwa uabadilishwaji wa figo yake, ambayo ilikua ikimsumbua, mwaka 2004 na iliyopelekea kustaafu kucheza mchezo wa raga.
Lomu enzi za uhai wake alichezea timu ya taifa michezo 73 kuanzia mwaka 1994 mpaka 2002 na kufunga mabao 43.
Anachukuliwa kama mmoja wa wachezaji nguli zaidi wa raga ya kimataifa.
Alifariki ghafla baada ya kurejea kutoka Uingereza ambako alikuwa ameenda kufanya kazi ya kupigia debe Kombe la Dunia la Raga lililomalizika majuzi.
No comments:
Post a Comment